WAONDOLEWA PORINI KISA BOMOA BOMOA GEITA
| Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi |
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
Wilaya ya Geita kwa kushirikiana na wakala wa Huduma za Misitu wameanza
operesheni ya kuwaondoa kwenye maeneo ya hifadhi za misitu wananchi waliovamia
maeneo hatari ya mlima wa Geita.
Wananchi zaidi ya 1,000 wameathirika
na bomoabomoa hiyo iliyoanza leo Ijumaa saa tatu asubuhi.
Akizungumza katika eneo hilo Mkuu wa
Wilaya ya Geita, Herman Kapufi amesema serikali ya wilaya imetimiza agizo
la kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa cha Oktoba mwaka jana
kilichotangaza wananchi hao wahamishwe katika maeneo hayo.
Wakizungumza na waandishi baadhi ya
wananchi balozi wa eneo hilo Cleofas Vitalis amesema wanaishi katika eneo hilo
toka mwaka 2002 na walinunua maeneo kutoka kwenye uongozi wa Mtaa wa Mkoani
ambao zamani kilikua Kitongoji cha Mkoani.
Amesema wamepewa taarifa ya kutakiwa
kuhama maeneo hayo miezi miwili iliyopita lakini hawakuhama wakiamini Serikali
itawahurumia kwa kuwa hawana pa kwenda na tayari wana watoto wanaosoma katika
Shule ya Msingi Mkoani.
Wanafunzi zaidi ya 100 wanaosoma
Shule ya Msingi Mkoani wameathiriwa na bomoabomoa hiyo.
Comments
Post a Comment