Wanafunzi 7 wafariki dunia katika mkasa wa moto Shule ya Sekondari, Nairobi
Takribani wanafunzi 7 wamefariki dunia huku wengine 10 wakijeruhiwa
kufuatia moto uliozuka saa nane za usiku katika bweni la shule ya wasichana ya Moi
mjini Nairobi,nchini Kenya
Akizungumza na vyombo vya habari
nchini Kenya waziri wa Elimu Dr,Fred
Matiang'i amethibitisha kuzuka kwa moto huo na kudai kuwa chanzo cha moto
huo bado hakijajulikana lakini tayari idara zote muhimu za uchunguzi zimewasili
shuleni hapo kubaini chanzo cha moto huo.
Majeruhi kumi wakiwemo wawili
mahututi wamekimbizwa katika hospitali ya Kenyatta mjini humo.
Aidha serikali imetoa salamu za pole
na rambirambi kwa wazazi waliopoteza watoto wao katika mkasa huo ulioikumba
shule hiyo na kuahidi kushirikiana nao katika kipindi hiki kigumu.
Shule hiyo imefungwa kwa majuma
mawili kufuatia mkasa huo.
Comments
Post a Comment