WAAMKA USIKU WA MANANE
KUSAKA HUDUMA YA MAJI.
| hivi ndivyo lilivyokubwa tatizo la uhaba wa maji |
Wananchi wa kijiji cha
Kasera kata ya Nyakaliro halmashauri ya Buchosa wamelazimika kuamka usiku wa
manane kusaka huduma maji baada ya
vyanzo vya maji walivyokuwa
wakitumia kukauka.
Wakizungumza na Radio sengerema
baadhi ya wanawake wa kijiji hicho wamesema wanapata shida kupata maji na
inawalazimu kuamka usiku wa manane kutafuta maji jambo linalopelekea upotevu wa
vyombo pamoja na vitisho mbalimbali.
Naye diwani wa kata hiyo Mh, Kalunga Ibrahim amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo katika
vijiji mbalimbali vilivyopo katika kata
yake licha ya kuwepo chanzo cha
maji kinachosambaza maji kwenda kata ya
Nyehunge.
Kwa upande wake
mbunge wa Jimbo la Buchosa Dkt,
Charles Tizeba kupitia mkutano wake wa hadhara na wananchi wa kijiji hicho
amesema haitafika mwaka 2020 kijiji
hicho kitakuwa na umeme.
Na Elisha Magege.
Comments
Post a Comment