Uhuru Kenyatta apinga uamuzi wa mahakama
Aliyekuwa
Rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta
,ametoa msimamo wake juu ya uamuzi wa mahakama uliotolewa leo wa kurudiwa kwa
uchaguzi wa urais, na kusema kuwa hakubaliani nao ingawa anaheshimu uamuzi huo.
Akizungumza
katika Ikulu ya Kenya muda mfupi baada ya uamuzi wa mahakama kutolewa, Uhuru
Kenyatta amesema anaheshimu uamuzi uliotolewa na mahakama wa kufuta matokeo ya
uchaguzi yaliyompa ushindi, lakini hakubaliani na uamuzi huo.
Pamoja na
hayo Uhuru Kenyatta amesema kwa kuwa wanaheshimu uamuzi wa mahakama, wako
tayari kurudi kwenye kampeni na kupiga kura tena kama ambavyo mahakama imetaka.
Leo
asubuhi Makama ya juu zaidi ilitoa uamuzi wa kesi ya uchaguzi iliyofunguliwa na
muunganiko wa vyama vya upinzani nchini Kenya (NASA) dhidi ya Tume ya Uchaguzi
iliyosimamia uchaguzi huo ambao Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi, na kuamua
kufuta matokeo hayo huku ikitaka urudiwe baada ya siku 60.
Comments
Post a Comment