UGONJWA WASHAMBULIA ZAO LA MUHOGO
| picha ya zao la muhogo |
Wakulima wa zao la muhogo wametakiwa kulima kwa
kufuata ushauri wa watalaamu wa kilimo ili kumaliza tatizo la ugonjwa wa zao
hilo.
Hayo yamebainisha na
Afisa kilimo wa kata ya Katwe katika Halmashauri ya Buchosa wilayani
Sengerema mkoani Mwanza Tumaini William
wakati akizungumza na Radio Sengerema ofisini kwake na kusema kuwa baadhi
ya wakulima wamekuwa wakilima
zao hilo
bila kufuata kanuni na taratibu za uendeshaji
wa kilimo hali iliyopelekea
kushuka katika uzalishaji wa zao
hilo.
Aidha William
ameongeza kuwa tatizo la ugonjwa wa
muhogo kanda ya ziwa ni mkubwa kwa mujibu wa tafiti za watalaamu wa
chuo cha kilimo cha Ukiliguru na tiba yake ni kuzingatia maelekezo ya maafisa ugani .
Na Charles Sungura
Comments
Post a Comment