RUNGU LA KIPOLE LATUA
KWA WAVUVI HARAMU
| nyavu haramu zikiwa zinachomwa |
Mkuu wa wilaya ya
Sengerema Mkoani Mwanza Mh, Emmanuel
Kipole amewataka viongozi pamoja na wananchi wanaojihusisha na uvuvi haramu
kuacha mara moja shughuli hiyo ndani ya ziwa Victoria.
Katika mahojiano na
Radio sengerema Mh,Kipole amesema zoezi la kupambana na uvuvi haramu
linaendelea na kwamba kiongozi yeyote atakaebainika kushirikiana na wavuvi
harama hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Hata hivyo Mh, Kipole
amesema changamoto kubwa inayowakabili
ni wavuvi wa maeneo mengine kuingia katika ziwa la upande wa wilaya ya
Sengerema na wanapowaondoa hukimbilia maeneo mengine.
Aidha Mkuu wa wilaya amesema ni wakati
muafaka wa wananchi wote wilayani Sengerema kuachana na uvuvi haramu katika
ziwa Victoria ili kulinda mazalia ya samaki.
Na Elisha Magege.
Comments
Post a Comment