RAIS MAGUFULI AWATAKIA SIKUKUU YA
IDD EL HAJJ NJEMA
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli, amewatakia
waumini wa dini ya Kiislam sikukuu njema ya Eid El Hajj.
Katika
ukurasa wake wa twitter Rais Magufuli ametoa ujumbe huo wa kuwatakia Eid njema,
huku akihimiza kudumisha amani, upendo na mshikamano.
Waumini wa
dini ya Kiislam nchini leo wanaungana na Waislam wenzao wote duniani,
kusherehekea sikukuu ya Eid El Hajj ambayo
huadhimishwa kila mwaka, mara baada ya ibada ya Hija kukamilika, na mara nyingi
husherehekewa kwa kuchinja wanyama waliohalalishwa kwa binadamu.
Comments
Post a Comment