ONYO LATOLEWA KWA
WAMILIKI WA NYUMBA
![]() |
| nyumba |
Wamiliki wa nyumba za
kupangisha Wilaya ya Sengerema wametakiwa kuwatambua mabalozi wa maeneo yao kwa
kuwapatia taarifa mapema
wakati wanapopata wapangaji na wageni katika nyumba
zao.
Tamko hilo limetolewa
na mwenyekiti wa kata ya Nyatukara Bwn,Pelana Bagume wakati alipokuwa kwenye kikao cha ulinzi na
usalama ambapo amewatahadharisha wamiliki ambao watabainika kuishi na mpangaji
bila kumtambulisha kwa kiongozi wa
mtaa watachukuliwa hatua kali pamoja na
mpangaji wake.
Kwa upande wake
diwani wa Kata ya Nyatukara Mh, salleh msabah amewatahadharisha wamiliki wa nyumba kuwa
kutowatambulisha wapangaji wao kwa viongozi wa maeneo yao ni kosa kisheria
hivyo watakaobainika watachukuliwa hatua
za Kisheria .
Na Said Mahera.

Comments
Post a Comment