MATUNDA YAANZA KUONEKANA BAADA YA KUKOMESHA UVUVI HARAMU
Imeelezwa kuwa baada ya
serikali kukomesha uvuvi haramu upatikanaji wa samaki Wilayani Sengerema umekuwa
mzuri huku wanunuzi wakielezea jinsi
wanavyopata samaki wakubwa tofauti na hapo awali.
Wakiongea na radio
sengerema wafanyabiashara wa samaki katika soko la migombani wilayani Sengerema
wamesema kwa sasa bei ya samaki mkubwa zaidi ni Tsh 25,000/= huku samaki wa
kawaida wakiuzwa sh,6000/= mpaka sh,2000/=
Hata hivyo radio
sengerema ikapiga hodi kwa wafanyabiashara wa dagaa ambapo wameelezea jinsi
bei ya biashara hiyo kupanda hadi kufika
kisado kuuzwa tsh 9000/= wakati awali kiliuzwa kwa tsh 5000/=huku wakieleza
changamoto wanazokumbana nazo wakati wa
uchuuzi wa biashara hiyo kwa wanunuzi.
Kwa upande wao wanunuzi
wamesema kuwa wanaipongeza serikali kwa juhudi wanazofanya juu ya wavuvi
wanaovua mazalia ya samaki kwa kuwa sasa wanakula samaki wakubwa.
Comments
Post a Comment