MATUMIZI MABAYA YA SILAHA YAWAFIKISHA MAKAMANI WATU 3
| SILAHA ZA MOTO |
Watu watatu
wamefikishwa katika mahakama
ya wilaya ya
sengerema mkoani mwanza
kwa tuhuma ya
makosa matatu ya
unyangh’anyi wa kutumia
silaha pamoja na
kusababisha maumivu ya
mwili.
Akisoma mashitaka
yanayowakabili mbele ya hakimu
wa
mahakama hiyo BI
MONIKA NDYEKOBORA .mwendesha mashitaka
wa jeshi la
polisi INSPECTA SLIVESTA
MWAISEJE,amewataja washitakiwa kuwa
ni JUMA KIFONGONYO mwenye umri
wa miaka 41
mkazi wa Lushamba, MTAKI
LYOMA maarufu LUBALAZA mwenye umri
wa miaka 45
mkazi wa Nyamatongo
na JASTINE MTESIGWA mwenye umri
wa miaka 40
mkazi wa Kamanga.
INSPECTA MWAISEJE
,amesema kuwa washitakiwa
wote kwa pamoja
wanashitakiwa kwa makosa matatu
ambapo kosa la
kwanza ni unyangh’anyi
wa kutumia silaha
kinyume na kifungu
namba 287 (A) cha
kanuni ya adhabu sura
ya 16,kuwa washitakiwa
wote kwa pamoja
wanashitakiwa mnamo agost 22
mwaka huu majira
ya saa 7:30 usiku
huko katika kijiji
cha nyamatongo wilayani
sengerema mkoani mwanza
waliiba kiasi cha
shilingi milioni moja
mali ya SIMONI
JOHN SANGIJA kabla na baada
ya kufanya unyangh’anyi huo
walitumia silaha aina
ya panga na
nondo katika
kufanikisha unyangh’anyi huo.
Kosa la
pili ni unyangh’anyi
wa kutumia silaha ,
kinyume na kifungu
namba 287 (A) cha
kanuni ya adhabu sura
ya 16,kuwa washitakiwa
wote kwa pamoja
wanashitakiwa mnamo tarehe
tajwa majira ya
saa 7:40 usiku huko
katika kijiji cha
nyamatongo wilayani sengerema
mkoani mwanza waliiba
kiasi cha shilingi
milioni moja na laki
tano mali ya MASHILA
MALULA kabla na baada
ya kufanya unyangh’anyi huo
walitumia silaha aina
ya panga na
nondo katika
kufanikisha unyangh’anyi huo.
Kosa la
tatu ni kusababisha
maumivu ya mwili
kinyume na kifungu
namba 225 cha
kanuni ya adhabu sura
ya 16,kuwa washitakiwa
wote kwa pamoja
wanashitakiwa mnamo tarehe
tajwa majira ya
saa 7:50 usiku huko
katika kijiji cha
nyamatongo wilayani sengerema
mkoani mwanza walisababisha maumivu
makali ya mwili
kwa KULWA WILIAMU MASABA kwa
kumkata na panga
kichwani na sehemu
mbalimbali za mwili
wake.
Hata hivyo
washitakiwa wote kwa
pamoja wamekana kutenda
makosa hayo na
watuhumiwa wamerudishwa rumande
hadi septemba 26
mwaka huu kesi
hiyo itatajwa kwa
maelezo ya awali
mahakamani hapo.
Na Joyce Rollingstone.
Comments
Post a Comment