MAHAKAMA
NCHINI KENYA YATENGUA USHINDI WA RAIS UHURU KENYATTA

Mahakama
ya juu nchini Kenya imefuta ushindi wa Rais Uhuru Kenyata kwa uchaguzi
uliofanyika Agosti 8, 2017, na kutaka uchaguzi huo urudiwe.
Hukumu
hiyo imetolewa leo na jopo la majaji 6 ilirushwa moja kwa moja kwenye vyombo
vya habari nchini Kenya, imesema uchaguzi huo utarudiwa baada ya siku 60.
Akisoma
uamuzi huo Jaji Mkuu David Maraga amesema tume ya uchaguzi ilikiuka Katiba na
Sheria katika baadhi ya mambo na hivyo kuathiri matokeo ya uchaguzi.
"Uchaguzi
wa urais uliofanyika Agosti 8 mwaka 2017, haukuandaliwa kwa mujibu wa katiba na
sheria hivyo matokeo yake ni batili. Natangaza kwamba Bw Kenyatta hakuchaguliwa
na kutangazwa kwa njia inayofaa, agizo linatolewa na kuagiza Tume ya Uchaguzi
kuandaa na kufanyisha uchaguzi mwingine kwa kufuata katiba na sheria katika
kipindi cha siku 60", alisema
Jaji Maraga.
Kesi hiyo
ilianza kusikilizwa Agosti 26 mwaka 2017 baada ya Muunganiko wa vyama vya
upinzani nchini Kenya (NASA) kuishtaki Tume ya Uchaguzi kufanya udanganyifu juu
ya uchaguzi huo uliompa ushindi Uhuru Kenyata.
Comments
Post a Comment