| Madawa ya kulevya |
MAPAMBANO YA DAWA ZA KULEVYA YANAENDELEA.
Mkuu wa wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza Mh, Emmanuel Kipole amewataka wananchi wote kutoa ushirikiano ili kutokomeza biashara na matumizi ya dawa za kulevya wilayani Sengerema .
Akizungumza na radio
Sengerema Mh, Kipole amesema tangu zoezi la kupinga marufuku matumizi pamoja na
biashara hiyo ya dawa za kulevya nchini Wilaya ya
Sengerema wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kudhibiti matumizi ya dawa hizo na
kilimo cha bangi.
Katika hatua nyingine Mh,kipole
amesema ni vyema wananchi wote kwa pamoja wakashirikiana kutokomeza biashara ya
dawa za kulevya, ili kuondoa vijana tegemezi kataka jamii.
Hivi karibuni Serikali ya awamu ya tano imepiga maarufuku biashara na matumizi ya dawa za kulevya nchini kwa lengo la kuwaokoa kundi kubwa la vijana waliokuwa wametumbukia katika janga hilo.
Na Elisha Magege.
Na Elisha Magege.
Comments
Post a Comment