MAAMUZI YA KESI YA URAIS NCHINI KENYA LEO KUJULIKANA
Muungano huo wa NASA unadai
kuwa matokeo ya uchaguzi ya mwezi Agusti yalikuwa na udanganyifu.
Tume ya taifa ya Uchaguzi
nchini humo ilimtangaza Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa uchaguzi kwa ushindi wa
zaidi ya nusu ya kura zote zilizopigwa na kumshinda mpinzani wake mkubwa,
mkongwe wa siasa za upinzani Raila Odinga.
Muungano wa upinzani nchini
Kenya unaitaka mahakama kuu kubatilisha matokeo hayo ya uchaguzi wa mwezi
uliopita.
Unadai kuwa mitambo ya Tume ya
Taifa ya Uchaguzi IEBC ilidukuliwa na matokeo kuvurugwa.
Upinzani pia unaituhumu Tume ya taifa
ya Uchaguzi kwa kutumia namba za kupigia kura ambazo zilikuwa hazijathibitishwa
rasmi.
Mahakama inayosikiliza kesi
hiyo imeruhusu tayari mawakili wa upinzani kuweza kupata Data na vifaa
vilivyotumika katika uchaguzi.

Comments
Post a Comment