KOREA KUSINI YAIJIBU KOREA KASKAZINI
KWA KUFANYA MAJARIBIO YA MAKOMBORA.

Korea Kusini imefanya mazoezi ya
makombora yake kuashiria shambulizi dhidi ya Korea Kaskazini, kujibu jaribio la
sita la nyuklia lililofanywa na Korea Kaskazini.
Mazoezi hayo yalihusu kurushwa kwa makombora ya masafa
marefu kutoka kwa ndege za kivita na ardhini.
Hii ni baada ya waziri wa ulinzi wa Marekani James Mattis
kuonya kuwa tisho lolote kwa Marekani au washirika wake kutoka Korea Kaskazini
litajibiwa vikali kijeshi.
Korea Kaskazini ilisema kwa ilifanyia jaribio bomu la
haidrojeni linaloweza kuwekwa kwa kombora la masafa marefu.
Korea mara kwa mara imekiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa na
shinikzo za kimataiafa ya kuitaka iachane na mpango wake wa zana za nyuklia.
Ndani ya miezi mwili iliyopita, Korea Kaskazini imefanya
majaribio ya makombra ya masafa marefu na hata kurusha kombora kupitia juu ya
anga ya Japan hadi bahari ya Pacific.
Baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa litafanya mkutano wa
dharura leo kujadili jibu la hatua hiyo ya Korea Kaskazini.
Comments
Post a Comment