KAA LA MOTO LAWASHUKIA WASIOWAPATIA MIKATABA WAAJIRIWA WAO
| Ongeza kichwa |
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mh Emmanuel Kipole
Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh Emmanuel Kipole amewataka waajiri wote wilayani Sengerema kuwapatia mikataba watumishi wao wa kazi.
Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh Emmanuel Kipole amewataka waajiri wote wilayani Sengerema kuwapatia mikataba watumishi wao wa kazi.
Amesema
hayo kufuatia kupokea malalamiko mengi kutoka kwa baadhi ya wananchi ambao
hawajapewa stahiki zao na kuwaomba wananchi kutambua haki zao za msingi pindi wanapoomba
ajira ili wapewe msaada wa kisheria pindi inapobainika kuwepo kwa tatizo la kutolipwa
stahiki zao ili kuepuka kudhulumiwa.
Mh. Kipole amesema kuwa waajiri na waajiriwa wanatakiwa kujua
sheria ya kazi ili kuweza kutekeleza majukumu kati ya mwajiri na mwajiriwa.
Hata
hivyo jamii imetakiwa kuzingatia suala la mkataba pale wanapopata ajira ili
kuepuka adha inayoweza kutokea.
Na Anna Elias.
Comments
Post a Comment