ELIMU YATAKIWA ZAIDI
KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI
| mifugo |
Wafugaji na wakulima
wa kijiji cha Ngoma Kata ya Igalula wilayani Sengerema mkoani
Mwanza wametakiwa kuunda vikundi ili serikali iweze kuwasaidia kuwa na
ufugaji wenye tija.
Hayo yamebainishwa na Afisa kilimo na mifugo wa
Kata ya Igalula Bwn, Stanley Shija
alipoongea na redio Sengerema ofisini kwake na kusema
wafugaji wakiungana kwa pamoja
watafanikiwa.
Shija amesema maendeleo
katika shughuli yoyote yanapatikana kwa
kuwa na malengo na mpango kazi na kuzingatia ushauri wa watalaamu wa kilimo na
mifugo.
Katika hatua nyingine amewaomba wananchi kutokatishwa tamaa na
changamoto za kilimo ikiwemo suala
la hali ya hewa katika msimu wa
kilimo ambazo haziepukiki na zile za
pembejeo kwani serikali inajitahidi kuzipatia ufumbuzi.
| mkulima |
Aidha ameongeza kuwa serikali itaweza kuwahudumia
wakulima na wafugaji kwa kutoa elimu na
mitaji kwa wananchi walioko kwenye vikundi.
Na,Charles Sungura
Comments
Post a Comment