CHARLES TIZEBA AWAPONGEZA WANANCHI KWA KUJITOLEA KUFANYA SHUGHULI ZA KIMAENDELEO
Image result for PICHA YA TIZEBA
Waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Buchosa wilayani Sengerema Mh, Charles Tizeba amewapongeza viongozi na wananchi wa kata za Bupandwamhela na Kafunzo kwa jitihada walizo onesha katika uboreshaji wa miundo mbinu pamoja na vituo vya afya katika kata zao.
Pongezi hizo amezitoa katika mkutano wake wa hadhara wa kuwashukuru wananchi wa kata hizo kwa kuendelea kumuamini na kumpa kura katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2015.
Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Buchosa Mh, Idama Kibanzi amewapongeza viongozi wa vijiji vilivyotekeleza ujenzi wa zahanati kwani mpaka sasa vijiji vingi katika Jimbo la Buchosa vimeanza kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi.
Hata hivyo Madiwani wa kata hizo mbili  Mh,Dotto Fransis Bulunda wa kata ya kafunzo na Mh,Masumbuko Bupamba wa kata ya Bupandwa wamemushukuru mbunge wa jimbo hilo kwa jitihada anazo onyesha za kuwaunga mkono wananchi wa jimbo lake.
Aidha Mh, Tizeba amewataka viongozi wote wa vijiji kuhakikisha wanawahamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo na katika kata zote hizo mbili ameahidi mifuko ya saruji, matofari na mabati kwa lengo la kuwaungo mkono wananchi na viongozi wa kata hizo ili kuchochea maendeleo katika kata hizo.

Na Elisha Magege.




Comments

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WANAFUNZI WAONDOKANA NA ADHA YA KUTEMBEA UMBALI MREFU KUFUATA ELIMU KATIKA KIJIJI CHA ILEKANILO WILAYANI SENGEREMA.