ASIMAMISHWA KAZI KISA MIGOGORO YA ARDHI
| Kiwanja |
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela leo amesikiliza kero
mbalimbali za ardhi kwa wakazi wa wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza huku
akimsimamisha kazi ili kupisha uchunguzi mthamini wa ardhi wa halmashauri
ya Jiji la Mwanza.
Mthamini huyo aliyefahamika kwa majina ya Egbert Rwabukabwa ambaye
ni mthamini daraja la pili wa halmashauri ya Jiji la Mwanza amesimamishwa kazi
baada ya mkazi mmoja wa wilaya hiyo kudai kuwa kuna eneo lake ambalo
amemilikishwa mtu mwingine.
Kutokana na hilo mkuu wa mkoa wa Mwanza amemuagiza katibu tawala
kumsimamisha kazi mthamini huyo ili kupisha uchunguzi na kutoa rai kwa
watumishi wa idara ya ardhi kufanya kazi kwa uaminifu
Leo september 13 mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela
amesikiliza kero mbalimbali za wananchi wa wilaya ya Ilemela kutokana na kuwepo
kwa malalamiko mengi ya wananchi kuhusu ardhi.
Na Veronica Martine
Comments
Post a Comment