AROBAINI
ZA MTEKAJI SUGU ZATIMIA
| Ongeza kichwa |
Mponjoli Mwabulambo
Jeshi
la Polisi Mkoani Geita linamshikilia kijana Samson Petro (18) mkazi wa Katoro wilayani Geita kwa tuhuma za
kuteka watoto katika mikoa ya Arusha na Geita.
Akithibitisha
kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Kamanda wa polisi mkoani Geita, Mponjoli
Mwabulambo amesema kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi na
utakapokamilika atafikishwa Mahakamani.
Kamanda
Mwabulambo amesema kijana huyo alikamatwa usiku wa Septemba 2 usiku katika
nyumba ya kulala wageni ya Shitungulu iliyopo mji mdogo wa Katoro akiwa na
mtoto Justine Ombeni mwenye umri wa miaka miwili aliyetekwa Ijumaa siku ya Eid
El Haji mkoani Geita.
Amesema
mtuhumiwa alimficha mtoto huyo katika chumba namba 11 cha kulala wageni
iitwayo Shitungulu wakati akisubiri mpango wake wa kutaka alipwe shilingi
milioni nne na wazazi wa mtoto huyo Omben Mshana na Elizabeth Omben.
Na Veronica Martine.
Comments
Post a Comment