AFARIKI
DUNIA AKIOGELEA NDANI YA ZIWA VICTORIA
| picha ya ziwa victoria |
Mtu
mmoja amefariki na wengine watatu kunusurika wakati wakiogelea katika ziwa
Victoria katika kijiji cha Luchili kata ya Nyanzenda Halmashauri ya
Buchosa wilayani Sengerema.
Aliye
patwa na mauti hayo amejulikana kwa ya Thobias martine mwenye umri wa miaka 33
mkazi wa kitongoji cha kabapani kilichopo katika kijiji na kata ya Nyanzenda.
Chanzo
cha tukio imeelezwa kuwa Thobias pamoja na wenzake watatu walikuwa wakivua
samaki katika ziwa Victoria kwa kutumia ndoano
na ilipo fika jioni waliamua kutoka ziwani kwa kuogelea kutoka kwenye
jiwe ambalo walikuwa wakilituimia kuvulia samaki na kuelekea nchi kavu ndipo
Thobias alipo zidiwa na maji na khari hiyo ikamsababishia kuzama.
Baraka
Pascal mwenye umri wa miaka 16,David Hamli miaka 17 na mwingine aliye fahamika kwa jina moja la Charles
mwenye umri wa miaka 13 ni wahanga wa tukio hilo na hapa wanasimlia njisi tukio hilo ambavyo
limetokea.
Happyness Deus ni mke wa marehemu na hapa anaelezea njisi mumewe
alivyo ondoka nyumbani na kuelekea katika shughuri zake za kila siku.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho Ibrahimu Mbata amedhibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kuwataka maafisa Uvuvi kutoa elimu kwa wavuvi ili wavuvi watambue mambo mhimu wanayo paswa
kuzingatia kabla hajaingia katika shughri zao za uvuvi
Na
Katemi Lenatus.
Comments
Post a Comment